CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimehoji matumizi ya helikopta ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), siku ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Kalenga, Jumapili ijayo.
Mratibu
wa Kampeni za CCM katika jimbo hilo, Miraji Mtaturo, aliitaka Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutoa msimamo kuhusu tangazo la Chadema kuwa
watatumia helikopta siku ya kupiga kura.
“Mwenyekiti,
wenzetu Chadema wametangaza kwamba siku ya uchaguzi, wataleta watu
zaidi ya 1,000 wakiwemo wabunge wao kulinda kura, lakini pia wamesema
watatumia helikopta yao kufanya doria, hiyo haiwezi kuwa doria itakuwa
ni kampeni,” alisema.
Mtaturo
alisema matumizi ya helikopta hiyo ni kinyume na Sheria ya Uchaguzi
inayokataza vyama kufanya kampeni siku ya uchaguzi, na pia akataka kujua
kama vyama vya siasa vinaruhusiwa kuweka vikundi vyake vya ulinzi
karibu na vituo vya kupigia kura.
Akijibu
hoja hiyo, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema
ni muhimu kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo vikazingatia
sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.
Jaji
Lubuva alisema hayo katika mkutano wa Nec na viongozi wa vyama vya
siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo, uliofanyika jana katika ukumbi
wa Siasa ni Kilimo, mjini hapa.
Hata
hivyo, hakufafanua kama ni makosa au la kutumia helikopta siku ya
uchaguzi. Chombo hicho ni cha usafiri kama ilivyo gari, pikipiki au
baiskeli, ambavyo havizuiwi na sheria kutumia siku ya kupiga kura
Kwa
kawaida, hata magari yaliyokuwa yakitumika wakati wa kampeni, siku ya
uchaguzi yanaruhusiwa kutumika lakini bila vipeperushi au alama yoyote
ya mgombea.
Helikopta kisiasa
Hata
hivyo, pamoja na kuwa helikopta imekuwa ikitumika kama nyenzo ya
usafiri, katika siasa za Tanzania imekuwa ikitumika kama nyenzo ya
kukusanya vijana na wasikilizaji katika mikutano ya kampeni.
Hilo
linadhihirisha na matumizi ya helkopta za kisiasa kupaa kutoka katika
kiwanja kimoja kwenda katika kiwanja kingine kilicho umbali usiozidi
kilometa moja, kusindikiza maandamano na hata kuvutia watazamaji kwa
kusimama angani.
Walinzi wa chama
Katika
hatua nyingine, Jeshi la Polisi limeahidi kuwakamata na kuwafungulia
mashitaka walinzi wa vyama vya siasa watakaonekana kuzagaa karibu na
vituo vya kupigia kura.
“Kazi
ya Polisi ni pamoja na kuhakikisha amani inakuwepo wakati wa upigaji
kura na utangazaji wa matokeo; sitaki kusikia habari ya vikundi vya
ulinzi vya CCM Green Guard na Chadema Red Brigade,” alisema Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi.
Uchaguzi
huo utakaofanyika Jumapili Machi 16, mwaka huu unahusisha vyama vitatu
vya siasa; CCM ambayo imemsimamisha Godfrey Mgimwa, Chadema Grace
Tendega na Chausta Richard Minja.
Vituo vya kura
Pia
Lubuva aliwataka wananchi kuondoka katika vituo vya kupigia kura mara
baada ya kupiga kura kwani kazi ya kulinda na kuhesabu kura itafanywa na
mawakala wa vyama pamoja na maofisa wa Tume
>>Habari Leo
>>Habari Leo
0 comments:
Post a Comment