WAISLAM WENYE ITIKADI KALI WAHUKUMIWA JELA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUUA NCHINI UINGEREZA


Gemini Donnelly-Martin, 20, na mama yake Amanda (kulia) wakiongea na Adebolajo wakati Ingrid Loyau-Kennett (kushoto) akiongea na Adebowale. Pembeni kushoto ni mwili wa Lee Rigby baada ya kuuawa.

Lee Rigby enzi za uhai wake akiwa na mpenzi wake Aimee West.
Magari  yakiwapeleka wafungwa hao gerezani.
Mtoto pekee wa marehemu.
Waandamanaji wakiwa nje ya mahakama wakati wa hukumu hiyo.
 
Michael Adebolajo.

 
Michael Adebowale.

 
Marehemu Lee Rigby.
WAISLAM wawili wenye itikadi kali nchini Uingereza, Michael Adebolajo na Michael Adebowale walitiwa hatiani Desemba mwaka jana na kuhukumiwa vifungo virefu kwa mauaji ya Lee Rigby huko Woolwich Barracks, kusini-mashariki mwa jiji la London mnamo Mei mwaka jana.
Waingereza hao weusi waliozaliwa nchini humo, walihukumiwa majuzi katika mahakama ya Old Bailey ambako walianzisha vurugu baada ya hukumu hiyo kwa kupiga kelele za  'Allahu akbar'  (Mungu Mkubwa) huku wakiwashambulia askari wa magereza.
Adebolajo (29) alihukumiwa kifungo cha maisha na Adebowale (22) amehukumiwa kifungo cha miaka 45 ikiwa na maana atatoka gerezani akiwa na umri wa miaka 67.
Watu hao walimshambulia Rigby wakati akitembea mtaani na  kumkatakata kwa silaha  hadi kufa, yote hayo yakifanyika mbele ya watu waliokuwa wamepigwa butwaa.
Washambuliaji hao walidai kuwa walikuwa ‘askari wa Mungu’ na walifanya hivyo kutokana na matatizo wanayoyapata Waislam wengine walio nchi za nje na kwamba walikuwa hawajutii kitendo hicho.
Kutokana na vurugu zao walizofanya mahakamani kwa kumrushia maneno hakimu, askari waliwatoa nje na hivyo hukumu yao kutolewa wakiwa hawamo mahakamani.
Miongoni mwa maneno waliyoyasema ni: “Wewe (Uingereza) na Marekani kamwe hamtakuwa salama.”

(DAILY MAIL)

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini