
Hili ni kama hitimisho la mada yetu, ile tuliyojadili kuhusu chanzo hasa cha watu wazima kujihusisha kimapenzi na watoto wa shule, hasa wa sekondari na vyuo. Kama ilivyotokea wiki iliyopita, idadi ya wadau waliowasiliana na mimi ilikuwa kubwa na uchangiaji wao wa mada ulikuwa ni wa kupendeza kabisa.
Kama ilivyokuwa awali, bado lawama zilielekezwa kwa pande zote mbili, yaani wapo waliowalaumu vijana wa shule na wale watu wazima. Mtakumbuka tulijaribu kuuliza ni kitu gani kifanyike, ambacho kwa maoni yenu kinaweza kupunguza tabia hii, kama siyo kumaliza kabisa.
Ingawa kila mmoja alijitahidi kushauri vile anavyoweza, lakini kwa ujumla watu wote walielekea kuamini kuwa endapo tamaa ikiepukwa, ya kihali na kimwili, kati ya wanafunzi na watu wazima, tatizo hili linaweza kupungua kwa kiwango kikubwa.
Watoto wa kike wakiondoa tamaa za maisha mazuri na kupata vitu vinavyowazidi umri, kama vile simu za bei mbaya na wazazi nao wakiamua kudhibiti tamaaa zao za mwili, upo uwezekano wa kuondoa tatizo hili.
Utandawazi nao umechangia sana watu kubadili aina ya maisha tunayoishi. Tofauti na zamani, ambapo mtoto mdogo alikuwa ni mali ya jamii husika, sasa hivi jukumu la kulea na aina ya maisha limeachwa kwa mzazi. Ndiyo maana wakati wapo baadhi ya watoto wanamiliki simu za bei mbaya walizonunuliwa na wazazi wao, wapo wanafunzi ambao hawatakiwi, siyo tu kumiliki, bali kukutwa na chombo hicho cha mawasiliano wakiwa bado shule.
Hata wazazi nao, hawaonekani kuvutiwa na ule msemo wa mtoto wa mwenzio ni wako pia, wanawakuza wa wenzao na kujisikia fahari kutembea nao. Mtu mmoja alipendekeza watu kumrejea Mungu, kwani mambo haya ya ukisasa, yametufanya sasa tusione haya kuwa na wapenzi ambao tumepishana sana.
Zifuatazo ni baadhi ya sms za wasomaji wengine na mapendekezo yao.
“Mimi ni dereva wa chuo kimoja cha Biblia, karibu yetu kuna shule moja ya sekondari, siku moja nilipokuwa natoka tu na gari niliwaona wanafunzi wawili wanaokaa nilikokuwa naelekea, nikasimama na kuwapa msaada, mmoja akaomba simu ampigie ndugu yake baada ya kuiona ndani ya gari, nikampa si akajibip, nikamuuliza mbona anajibip akasema mawazo sijui yalikuwa wapi, baada ya hapo alianza kunitumia sms mbalimbali, nilipogundua shida yake nikamtaka tukutane, unajua nilimpeleka kanisani na nikamwambia hapa ndio nyumbani kwetu, nikamtaka aokoke, nikamfanyia maombi, je kama ningekuwa sijaokoka!
Miye kwa maoni yangu tufanye hivi, ili tuweze kukomesha yule mtu anapokuwa gesti, yaani mapokezi inatakiwa awe anatazama umri wa mzee na denti mwenyewe, je huyu denti anaweza kweli kushea love na huyo mzee? Kama ataona haiendani hiyo love basi amwambie yule baba au denti mwenyewe kuwa hampaswi kuingia kwenye chumba, akikataa huenda hiyo itasaidia.
Kama nilivyochangia kuwa hili jambo ni Comprehensive sana, udhibiti wake unahitaji nguvu kubwa mno kwani uhuru mkubwa tulionao ambao umechangiwa na Globalization pamoja na social influence inakuwa si rahisi sana, ila tunapaswa tu kumrudia Mungu na kurejea maadili yetu ya kiasili. Nyorido H A, Kisongo Arusha.
Anko miye naona wazazi wawe makini na watoto wao, pia wanafunzi wajitambue, waache kujidhalilisha kwa watu wazima. Mwanafunzi unawezaje kuchanganya elimu na masomo? Jamani wanafunzi amkeni kuweni makini, magonjwa ni mengi sana na pia wanafunzi anaweza kuharibu maisha yake endapo atapata mimba na hao watu wazima huwa hawakubali hizo mimba.
Anko hili tatizo kiukweli siyo rahisi kama unavyodhani, kilichopo sisi wenyewe tuingiwe na ubinadamu kuwa mtoto wa mwenzio ni mwanao na baba wa mwenzio ni baba yako na siyo baba mkubwa wala mdogo, ni baba yako mzazi, hapo tutakapoonesha kizazi hiki na kijacho. Tofauti na hapo anko tuking’ang’ania baby, baby, tutakuja kukosa ushahidi kweli.
0 comments:
Post a Comment