NI
kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Fumanizi la aina yake
lilitokea juzikati asubuhi ya saa 2, Mtaa wa Mbwela, Tandika jijini Dar
ambapo mjamzito aliyejulikana kwa jina la Semeni alipata ‘kichaa’ cha
muda baada ya kumfumania mumewe, Dullah akiwa na mwanamke mwingine
chumbani kwao, Risasi Jumamosi lina kisa kizima.
Akisimulia
mkasa huo, Semeni mwenye ujauzito wa miezi 6 alisema kabla ya tukio
aligombana na mumewe akarudi kwao kwa muda wa siku mbili lakini walikuwa
wakiwasiliana mpaka asubuhi ya tukio ambapo alimpigia simu kumwambia
anafuata nguo kwa vile anakwenda kliniki.
“Nilipokuwa njiani nilimpigia simu mume wangu, nikamwambia nimekaribia, lakini akasema yeye amekwenda Posta.
“Nilipokuwa njiani nilimpigia simu mume wangu, nikamwambia nimekaribia, lakini akasema yeye amekwenda Posta.
“Pamoja na majibu hayo, niliamua kwenda. Nilipofika nilikuta mlango
umefungwa kwa ndani, nikampigia simu mume wangu, akasisitiza hakuna mtu,
yeye yupo Posta.
“Nilichungulia na kuona funguo, nikajua kuna mtu ila hataki kunifungulia, hapo wasiwasi ukazidi kwamba huenda kuna jambo linaloendelea,” alisema Semeni.
Mwanamke huyo aliendelea kuanika kwamba kufuatia hali hiyo aliwaita
majirani ambao ilibidi wamtishe mtu aliye ndani kwamba asipofungua
watavunja mlango, ndipo mlango ukafunguliwa na kumkuta Dullah akiwa na
mwanamke mwingine chumbani, lakini mumewe huyo alichoropoka na kukimbia.
“Nilishtuka, nikapiga kelele ya mshangao kutokana na kitendo alichokifanya mume wangu, kumleta hawara mpaka kwenye chumba tunacholala!
“Nilishtuka, nikapiga kelele ya mshangao kutokana na kitendo alichokifanya mume wangu, kumleta hawara mpaka kwenye chumba tunacholala!
“Sijaamini kilichotokea! Yule ni mume wangu, amewezaje kumleta
mwanamke ndani ya chumba tunacholala tena kuna wapangaji wenzangu
wameshuhudia,” alisema mwanamke huyo huku akilia machozi.
Akaendelea: “Mimi hapa nyumbani siachiwi hela ya kula, kila siku
nakula nyumbani kwetu, nikijua labda mume wangu hana, kumbe anamalizia
kwa hawara! Jamani inaniuma sana, kama hivyo bora amuoe basi tuje tuishi
wote au aniache akae yeye.”
Akizungumza na gazeti hili kwa uso ‘uliochunwa’, mwanamke aliyedaiwa
kufumaniwa, Mwanaidi huku akiwa ‘ametaitiwa’ ndani, alijitetea kuwa
hakufahamu kama Dulla ana mke.
“Mimi aliniambia hana mke wala mtoto na ndiyo maana nilikubali kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na yeye si vinginevyo, kama ningejua nisingekubali kuja, kwa hiyo siyo kosa langu,” alisema Mwanaidi.
Baada ya hali kutulia, baba mzazi wa Dullah ambaye anaishi jirani aliitwa kuamua ugomvi huo na kuamuru wote waende nyumbani kwake ambapo aliagizia gari.
Wawili hao walipofika nyumbani kwa mzazi huyo walimshusha Semeni na kumtaka atangulie ndani, alipoingia tu, nyuma dereva alitakiwa kuondoka gari hilo kwa kasi huku Mwanaidi akiwemo ndani ili kumnusuru.
Baada ya kubaini ‘triki’ hiyo, Semeni alijirusha chini kwa hasira na kujigalagaza kisha kulikimbiza gari hilo bila mafanikio.

0 comments:
Post a Comment