Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika
na kitu cha mlipuko katika eneo la mkunazini, na kuleta mtafaruku katika majira ya mchana..Katika mlipuko huo hakuna
mtu aliyepata majeraha na uharibifu wa majengo katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na
Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ ,
katika eneo la tukio na kutoa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa alipofika
katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika
eneo hilo wakati wa mlipuko huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda
wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuagalia na kuchunguza tukio hilo la
mlipuko katika eneo la Mkunazini
Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na
kitu kinachodhaniwa ni bomu, katika tukio hilo hakuna Mwananchi
aliyejeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment