Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akiangalia matembezi ya mshikamano wakati yakiingia
uwanjani kabla hajaanza kuhutubia wakazi wa Shinyanga mjini.
Wakazi wa Shinyanga
mjini wakiwa na Furaha ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao walikuwa
madiwani kwa kupitia Chadema ambao tarehe 25 walijiuzuru na tarehe 26
Februari 2014 kujiunga na CCM.
Zakaria Martin Mfuko
aliyekuwa Diwani wa Chadema Kata ya Masekelo akihutubia wakazi wa
Shinyanga mjini kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo na kuwaambia
wananchi hao ameamua kurudi CCM kutokana na ufisadi na ukiukwaji ya
maadili ya Uongozi ndani ya Chadema.
Sebastian Peter maarufu
kama Obama aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Ingokole akihutubia
wananchi kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akimsaidia kufunga vifungo vya shati Ndugu Sebastian
Peter aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ingokole ambaye amerudisha Kadi yake
ya Chadema na kupokelewa rasmi CCM kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo
mjni Shinyanga.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga mjini na
kuwaambia Huu ndio Mwanzo tu,aliwaambia CCM imejengwa kwa misingi imara
hivyo itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akimpa ushauri Mbunge wa Shinyanga Mjini Ndugu
Stephen Masele juu ya VETA mkoani hapo kutoa kozi zinazoendana na
mahitaji ya Soko la Viwanda vya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini tarehe
26 Februari 2014.
0 comments:
Post a Comment