wastara4
Jumatano ya wiki hii muigizaji mrembo wa Bongo Movie Wastara Juma, alikuwa mgeni katika kipengele cha ‘Kikaangoni Live’ ya EATV, ambayo mtu maarufu huchat live na mashabiki wake kupitia ukurasa wa EATV.


Urembo wa muigizaji huyo huenda ndio chanzo cha mishale mingi ya maswali kutoka kwa mashabiki wa Wastara, waliokuwa na kiu ya kutaka kufahamu baada ya kumpoteza mume wake Sajuki, hivi sasa ni mwanaume gani mwenye bahati ambaye yuko katika kisiwa chake cha ‘makopa’, yaani mpenzi wake wa sasa.
“Inshort mimi nina watoto watatu ambao wananiangalia wao zaidi kuliko kitu chochote” huo ndio ulikuwa mwanzo wa jibu la maswali hayo kutoka kwa Wastara.
“Kikubwa nachokifanya sasa hivi ni kuangalia watoto wangu na kuwawekea misingi mizuri kama kuna kitu ambacho nilimiss wakati niko kwenye matatizo na mpaka mume wangu kufariki , basi naangalia jinsi ya kukirudisha katika hali yake ya kawaida, lakini swala la mahusiano silipi kipaumbele”. Alisema Wastara alipozungumza na E-News ya EATV baada ya ‘Kingaangoni Live’.
wastaraeatv-2
Akizungumzia career yake ya uigizaji Wastara amedai kuwa mashabiki wake watarajie movie zake nyingi zitakazotoka mwakani , sababu kwa mwaka huu tunaoumaliza amefanikiwa kufanya filamu saba ndani ya miezi sita, kitu ambacho hakuwahi kufanya toka ameanza uigizaji.
“Mimi sijawahi kufanya movie hata mwaka mmoja toka nimeanza kufanya sanaa kama mwaka huu, nimefanya movie saba…ni movie nyingi sana kwangu, kwasababu sijawahi”. Alimaliza Wastara.
Kwa sasa movie mpya ya Wastara iliyoko sokoni inaitwa ‘Shaymaa’.