MASTER JAY AFUNGUKA "WASANII WA BONGO FLAVA NI WEZI"


Producer mkongwe na C.E.O wa MJ Records Master J amesema kuwa wasanii wa Tanzania wanawaibia watayarishaji wa muziki.

“Huwezi kuchukua wazo langu uende kulitumia kutengeneza hela halafu uniambie kwamba ‘bwana mimi sikupi kitu’, wasanii ni wezi tu Bongo.” Amesema Master J.


Unaweza kudhani labda aliteleza kidogo kusema hilo, lakini kwa kuwa ana uhakika na anachokisema, producer huyo mwenye mchango mkubwa kwa muziki wa kizazi kipya hapa nchini aliweka mkazo kwenye maneno yake.

“Watu wanaogopa kuongea, mimi ngoja niongee tu ukweli, wasanii wa Bongo ni wezi. Kitu wanachokifanya ni wizi. Unajua mwizi anakaaga kimya, lakini wanakwenda kwenye media wanaropoka ‘nimeingiza million 300 (kwa kutumikia haki ya Lamar bure na simpi kitu)’. Yaani unaiba halafu unaenda unatangaza kwenye media!” alifunguka Master J.

“Hata hawaogopi! Walivyokuwa hawajui kwamba sheria hairuhusu kufanya hivyo, na kiukweli akiamua kupania anapata cha kwake, sema tu maproducer hawafuatilii. Lakini wanavunja sheria kabisa na ni wezi. Huwezi kufanya hivyo halafu unaenda unatangaza, kaa kimya…kula na kipofu. Sio sawa wanavyofanya.” Aliongeza kwa msisitizo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini