Sara Mvungi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi jioni maeneo ya
Kwanyerere, Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo Sara alikuwa kwenye
bodaboda ghafla ilitokea nyingine ikiwa kwenye mwendo wa kasi na
wahusika walikuwa wawili ambao walimnyang’anya pochi.
Akizungumza kwa masikitiko, Sara alisema ndani ya pochi hiyo kulikuwa na simu mbili aina ya blackberry, fedha taslimu laki tatu,dola mia moja, vitambulisho na vitu vingine vingi.
“Nimeumia sana moyoni jamani sijui nianzie wapi ila namshukuru Mungu sijaumia nawaomba mashabiki na jamii kwa ujumla kuwa makini kwani bodaboda siyo watu wa kuaminika na huu mwisho wa mwaka ndiyo wizi umezidi,”alisema Sara.