Mh! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Riyama Ally, amejikuta akiwa njia
panda baada ya kutakiwa kunywa pombe ya kienyeji aina ya ugimbi ambayo
hajawahi kunywa maishani mwake.
Riyama aliingia kwenye mtihani huo juzikati pande za Songea alipokuwa
amekwenda kikazi ambapo alitakiwa kunywa pombe hiyo kutokana na matakwa
ya filamu lakini akashindwa.
“Ulikuwa mtihani kwa kweli, ili kuleta uhalisia ilitakiwa ninywe
pombe hiyo lakini kiukweli nilishindwa kwa kuwa sijawahi kunywa hata
siku moja, ilibidi nizuge na kopo tupu,” alisema Riyama ambaye ni mkali
wa kuzitendea haki sini za siriasi.
0 comments:
Post a Comment