Dar es Salaam, Katika kusheherekea sikuu ya Pasaka, wasanii Chege
Chigunda au mtoto wa Mama Saidi na mwenzake YP wametoa burudani ya aina
yake kwa wakazi wa Dar es Salaam katika tamasha maalum la Cheka
Bombastik lililofanyika katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam.
Burudani ilianza kwa staili ya aina yake kwa wasanii Chipukizi
“Underground” kupanda jukwaani na kutoa burudani kwa maelfu ya mashabiki
waliojitokeza katika fukwe hizo.
Uwanja ulikuwa hautoshi pale alipopanda jukwaani Chege Chigunda na
kuwapeleka Mashabiki wake Uswazi Take Away, kwa kuifanya kazi yake vyema
na kutoa burudani ya Kipekee kwa pamoja waliimba nyimbo kadhaa za
kundi la Wanaume Family.
Akizungumza na waandishi wa habari punde baada ya kumalizika kwa
Tamasha hilo, Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, ambao ndio
waandaaji wa Tamasha hilo, Matina Nkurlu amesema kuwa Imekuwa kawaida
kwa kampuni yao kutoa burudani kwa Wakazi wa Dar es Salaam na Sehemu
nyingine katika ziku za siku kuu.
“Umekuwa ni Utaratibu wetu wa kawaida wa kutoa burudani kwa
Watanzania ambao wamekuwa wakituunga mkono siku zote na kutufanya kuwa
namba moja kila siku,” alisema Nkurlu na kuongeza, Umati huu ni ishara
tosha ya namna wakazi wa Dar es Salaam walivyo kubali burudani hii”
“Burudani hii ni Maalum kwa wale wote ambao wanapenda kupumzika
katika sehemu za Fukwe kama Coco Beach, tunatambua kuwa kipindi hiki
wengi wanapenda kupumzika na familia zao hivyo ni vyema pia wakapata
burudani ya aina hii.” Alisema Nkurlu.
Meneja huyo alisema kuwa burudani hiyo ni ya siku mbili, siku ya
tarehe 20 na 21 ya Mwezi April ambayo ni jumapili na jumatatu ya pasaka,
na wateja wa Vodacom watakao jitokeza katika Tamasha hilo, watapata
zawadi mbalimbali na wataunganishwa na huduma ya Cheka Bombastik Bure,
Ili kuweza kupiga simu kwa bei nafuu.
“Tumefanya Tamasha hili tukiwa na ujumbe maalum kwa wateja wetu wa
Vodacom kuhakikisha wanajiunga na huduma yetu ya Cheka Bombastik ambayo
inawapa nafasi ya kuchagua bando za aina mbali mbali za kupiga simu,
Vodacom kwenda Vodacom au kutoka Vodacom kwenda mitandao mingine.”
Alihitimisha Nkurlu.
0 comments:
Post a Comment