Staa wa sinema za Kibongo, Jenifer Kyaka ‘Odama’.
HABARI njema! Staa wa sinema za Kibongo, Jenifer Kyaka ‘Odama’ amejifungua kidume huku akikataa kumtaja baba wa mtoto huyo.
anayedaiwa kwamba ni mheshimiwa serikalini.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Odama alijifungua kwa operesheni hivi karibuni kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar baada ya kuwa kimya kwa miezi kadhaa kutokana na likizo ya uzazi ambayo ilimfanya asimame kuigiza filamu kwa muda.
Jenifer Kyaka ‘Odama’ akiwa kwenye pozi.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti lilimtafuta kwa njia ya simu ambapo alikiri kujifungua mtoto wa kiume na kwamba anamshukuru Mungu kwani yeye na mwanaye wanaendelea vizuri.
“Namshukuru sana Mungu na mimi sasa naitwa mama. Hayo mengine ya baba mtoto tuyaache muda ukifika mtamuona,” alisema Odama.
0 comments:
Post a Comment