WEMA SEPETU AUMBUKA BAADA YA KUMDANGANYA PASTOR MYAMBA


Juzi kati Wema Sepetu alialikwa kama mgeni rasmi katika hafla ya chuo cha TFCT cha mafunzo ya filamu kinachomilikiwa na Emmanuel Myamba "Pastor Myamba" ambaye pia ni star wa filamu nchini. 

Wema alialikwa kwa shinikizo la wanafunzi wa chuo hicho sambamba na Jokate Mwegelo. Wema aliombwa mwanzoni kuhudhuria tukio hilo na kukubali, alipopigiwa simu hatua  za mwisho alisema hataweza kufika kwasababu amepata msiba wa shangazi yake. 

Lakini ikabainika kuwa Wema alimdanganya Myamba kwani hakukuwa na msiba wowote wa shangazi yake .Chanzo kimoja  kilicho karibu na Wema kilichozungumza na Globalpublishers, kilisema kuwa kama kungekuwa na tukio la msiba wangejua tu kwani Wema huwa hawafichi na siku hiyo walikuwa na ratiba ya kwenda kwenye tukio moja la starehe ambalo ratiba yake haikubadilika.

Baada ya tukio la Wema kuikaushia hafla hiyo ilibidi waandaaji wawaombe radhi wageni waalikwa wakiwemo waandishi wa habari....

Myamba alipotafutwa  na kuulizwa kuhusu tukio hilo alikiri na kusema amesikitishwa sana na Wema kwa alivyofanya kwani alialikwa kutokana na heshima aliyonayo.
 
"Nimemshangaa sana lakini mbona mwenzake Jokate alikuja, ni kwasababu anajitambua na ni professional." Alisema Myamba ambaye alipata umaarufu kwa kuigiza filamu nyingi na marehemu Steven Kanumba akicheza nafasi kama pastor.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini