VICTORIA KUTOKA NCHINI KENYA AMEDAI KUWA HANA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA DIAMOND

Msanii wa Bongo Flava hapa nchini Nasibu Abdul aka Diamond Platnumz aka Mr. Ngololo alikunusha tetesi za kuwa na mahusiano na mwimbaji kutoka pande za Kenya Victoria Kimani baada ya kukutana hivi karibuni Afrika Kusini.

Tetesi hizo zilikuja baada ya kupiga picha ya pamoja wakati walivyoungana na wasanii wengine wa kubwa wa Barani Afrika kwa ajili ya ‘One Campaign.

Victoria ambaye makazi nchini Nigeria na yeye ametoa yake baada ya kufanya mahojiano na Nairobi News alisema ” Mimi sijui hizo tetesi zimetoka wapi nimekutana na Diamond mara moja tu tulipokuwa tunarekodi wimbo wa pamoja wa One Campaign huko Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, pia sina namba yake na sijawahi kuwasiliana na nae toka tulivyokutana na Afrika Kusini.”

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini