Msemaji kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amesema kuwa rapper Lord Eyez amesimamishwa na kampuni hiyo kutokana na kuvunja maadili.
Nick wa Pili amesema baada ya kupokea taarifa za Lord Eyez
kushikiliwa na polisi huko Arusha kwa wizi wa Laptop walikaa kikao na
kuamua kumsimamisha.
“Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez
tumemsimamisha kazi kikampuni,”
“Uamuzi wa kumsimamisha tumeufikia jana na leo ndio tumeamua kutangaza rasmi kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi na amesimamishwa kutokana na misingi na makubaliano ya kampuni,kulingana na maadili ya kampuni yetu na mawazo yetu kwa pamoja ndio yamefanya tukamsimamisha. Kwahiyo ni kwamba tumemsimamisha kutokana na makubaliano ambayo yalifikiwa ndani ya kampuni ambayo mengine yatabakia ndani ya kampuni.” Nikki wa Pili

Uamuzi huo wa Weusi umekuja kufuatia taarifa kuwa Lord Eyez
alikamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa laptop Jumamosi, huko Arusha
na baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa
anatuhumiwa kwa wizi wa laptop aina ya ‘Dell’.
Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma
za wizi wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza
kumsamehe msanii huyo.
0 comments:
Post a Comment