Devota Mbaga
Katibu
Msaidizi wa Bongo Movie Unity, Devota Mbaga amezawadiwa gari aina ya
Toyota Harrier Lexus na mumewe aliyemtaja kwa jina la Mr. Mbaga baada ya
kudumu katika ndoa kwa muda wa miaka 20.
Akizungumza na Ijumaa, Devota alisema anamshukuru Mungu kwa kukaa
katika ndoa yake kwa amani na hatimaye kutimiza miaka hiyo kwani ni
wachache wanaotimiza umri huo.
Devota akipozi na gari lake alilozawadiwa.
“Siku niliyotimiza miaka hiyo nilikuwa nimejisahau lakini mume wangu
alithamini na kunishtukiza kwa kunizawadia gari ambalo aliliandika jina
langu kwenye kioo cha ‘sight mirror’ upande wa kushoto, namshukuru Mungu
na mume wangu pia,” alisema Devota.
0 comments:
Post a Comment