Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa kikifanya kampeni katika kijiji cha Kidamale Jimbo la Kalenga, kimelazimika kusitisha kampeni zake kwa muda ili kushiriki maziko ya watu watatu waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika jimbo hilo.
Ajali hiyo ilitokea juzi kwa kuhusisha gari la kiwanda cha kusambaza
maji ya Afrika cha mkoani humu aina ya Isuzu Foward lenye namba za
usajili T 750 AFJ.
Aidha, ajali hiyo pia ilisababisha watu wanne kujeruhiwa.
Waliokufa katika ajali hiyo ni Nyagile Luvanda (38), Sabasaba Kunzugala
(35) na Anskali Chengula (20), wote wakazi wa kijiji cha Kidamali.
Majeruhi ni Shukuru Msigwa (20), Riziki Kyando (30), Jimmy Luvanda (21)
na Spedito Mgongolwa (28), wote wakazi wa kiojiji cha Kidamali.
Majeruhi hao walipelekwa katika hospitali ya Tosamaganga kwa matibabu.
Akiongoza maziko hayo juzi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu
Nchemba, alisema CCM imepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na ndiyo
maana wamelazimika kusitisha kampeni hizo na kushiriki kwenye maziko.
Nchemba kwa niaba ya CCM alitoa Shilingi milioni moja kwa familia za
marehemu hao huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tawi la
Kidamali, waklitoa Sh. 50,000.
Miili ya marehemu hao ilizikwa katika makaburi ya kijiji cha Kidamali.
Aidha, Nchemba alisema kuwa endapo CCM itapewa ridhaa ya kuongoza katika
jimbo hilo, mgombea wao Godfrey Mgimwa, atasaidia watoto walioachwa na
marehemu William Mgimwa.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment