HAYA unaweza kuyaita ni maajabu ya mafuta ya samaki baada ya kuonesha uwezo wa kuponya hata ‘mfu’ aliyekwisha tangaziwa kifo na madaktari bingwa. Ni kisa cha kweli kilichotokea nchini Marekani hivi karibuni na kuoneshwa na Kituo cha Televisheni cha CNN ambacho kinaaminika na kutizamwa na mamilioni ya watu duniani.
Septemba 16, 2012 kijana mwenye umri wa miaka 16, Grant Virgin wa nchini Marekani aligongwa na gari na kuumia vibaya kiasi cha kupoteza fahamu na kuonekana hawezi tena kupona kutokana na majeraha aliyoyapata mwilini na hasa sehemu ya kichwa.
Madaktari walijitahidi kadiri ya uwezo wao kuokoa maisha yake, walifanikiwa kwa kiasi fulani, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo, waliwatangazia wazazi wake kuwa mtoto wao hatapona, labda angeweza kuishi kwa usiku mmoja tu.
Wiki mbili baada ya ajali hiyo, kijana Grant alikuwa bado amelazwa hospitalini hajitambui (in a coma) huku familia yake ikielezwa na madaktari kuwa hakuna wanachoweza kufanya zaidi ya kusubiri siku yake ya kufa ifike.
Grant Virgin.
Hata hivyo, wazazi wa Grant hawakukubaliana na maelezo ya madaktari, badala yake wakaanza kutafuta tiba mbadala kwa kujaribu kufanya kila aina ya ushauri waliopewa. Walijaribu tiba mbadala tofauti ambazo zilianza kuonesha matumaini kwa Grant kupata fahamu na kuanza kuongea maneno mafupi japo kwa taabu.
Wakati wakijaribu tiba hizo mbalimbali, siku moja mama yake Grant aliona habari moja CNN ikizungumzia uwezo wa mafuta ya samaki (Omega-3) katika kutibu uvimbe kichwani ambapo ilielezwa namna ambavyo mafuta hayo yanavyoweza kupunguza au kuzuia uvimbe kichwani.
Ingawa kulikuwa hakuna utafiti mkubwa wa kisayansi wa moja kwa moja unaoweza kuthibitisha hilo, lakini wazazi wa Grant walianza kumlisha mtoto wao kwa njia ya mrija mafuta ya samaki kiasi cha gramu 20 kwa siku. Siku mbili baadaye, kwa mshangao wa kila mtu, Grant akiwa kitandani hospitali, aliweza kumpigia simu mama yake na kuongea naye kwa kutamka sentesi kamili.
Awali alikuwa hawezi kuongea kwa sentesi kamili, alikuwa akiongea kwa taabu na kwa kukatisha na kurudia maneno, (nafikiri unajua mtu aliyepooza mdomo anavyoongea), lakini baada ya kutumia mafuta hayo kwa siku mbili tu aliweza kuongea kwa ufasaha, kiasi cha mama mtu kuona kama ni ndoto.
Aliendelea na dozi ya mafuta ya samaki na kila baada ya muda hali yake ikawa inaendelea kuimarika, alikuwa hawezi kukaa akaanza kukaa, alikuwa hawezi kusimama akaanza kusimama, alikuwa hawezi kutembea akaanza kutembea.
Hivi sasa, mwaka mmoja baadaye, ameweza kupona kabisa huku akifanya shughuli zake zote, ikiwa pamoja na kucheza michezo mbalimbali na kusababisha wataalam wa masuala ya tiba kufanya utafiti tena wa kina juu ya uwezo wa mafuta ya samaki ambayo siyo tu yanasaidia matatizo ya uvimbe kichwani, bali kwa mwili mzima.
Chanzo kizuri cha kirutubisho aina ya Omega 3 Fatty Acids ni samaki, hivyo watu wanashauriwa kula samaki. Hata hivyo, kutokana na uchafuzi wa mazingira, samaki wengi wameharibika na kukosa kirutubisho hicho muhimu.
Kwa kuzingatia hilo, inashauriwa watu kupata mafuta ya samaki kwa njia ya vidonge (food suplements) vinavyotengenezwa na makampuni yanayoaminika kimataifa katika utengenezaji wa bidhaa za vyakula kwa njia ya vidonge vyenye ubora wa hali ya juu.
0 comments:
Post a Comment