Tundu Lissu akiongea na wafanyakazi wa Global (hawapo pichani).
WAKATI Watanzania wote macho na masikio yao yakiwa Dodoma kwenye kikao cha Bunge la Katiba, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) bado kuna mgogoro unaoendelea kuunguruma chinichini.
Mgogoro huo kati ya uongozi wa Chadema na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Zuberi Kabwe umefunikwa na mjadala wa Katiba Mpya ya Nchi, lakini safu hii ilifanya juhudi ya kumleta ndani ya chumba cha habari cha Global Publishers, Bamaga Mwenge na ‘kumchimba’ Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ili kujua kile kilicho nyuma ya pazia kuhusiana na mgogoro huo.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki alifichua siri kwamba Kamati Kuu ya Chadema ilishafanya uamuzi wa kumtimua katika chama lakini ikakwama kufanya hivyo baada ya kuzuiliwa na Mahakama Kuu ambako Zitto amefungua kesi dhidi ya Chadema.
Mwandishi: Unadhani nini kimesababisha chokochoko zote hizi?
Lissu: Zitto alikuwa anataka uenyekiti wa chama chetu, siyo jambo baya, lakini alishiriki kutengeneza waraka wa siri, siri kubwa, ambao haukubaliki. Alimtuhumu mwenyekiti wetu kuwa hana elimu, malaya, mnunuzi mkuu wa mali za chama, fisadi na mambo mengine mengi ya namna hiyo. Huu ni uongo mkubwa, hatuwezi kuukubali.
Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers Ltd wakimsikiliza Tundu Lissu.
Mwandishi: Kuna madai kuwa Zitto amemkashifu mwenyekiti wenu, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa kuhusu ufisadi wa fedha za chama, unaweza kufafanua hayo?
Lissu: Ni vigumu kuzungumzia umalaya wa mwenyekiti wetu lakini nadhani hayo ni mambo ya chumbani ambayo kwa vyovyote huwezi kuyaunganisha na uongozi.
Hayo ni mambo binafsi, kama tungekuwa tunalinganisha mambo hayo, sijui tungesema nini kuhusu Rais Nelson Mandela na Bill Clinton wa Marekani ambaye alikumbwa na kashfa katika mojawapo ya vibaraza vya Ikulu ya White House. Zitto, akiwa Naibu Katibu Mkuu, anafahamu kuwa kila jambo linajadiliwa na Kamati Kuu ambayo yeye ni mjumbe na kwamba tuhuma zote dhidi ya mwenyekiti na katibu mkuu ni uongo.
Mwandishi: Ina maana sasa Zitto nyinyi hamumtambui kama mbunge wenu?
Lissu: Hatumtambui, sasa mbunge huyo ambaye ni wa Jimbo la Kigoma Kaskazini amebakia kuwa mbunge wa mahakama baada ya Januari mwaka huu Mahakama Kuu ya Tanzania kutuzuia Chadema kujadili hatima ya uanachama wake.
...Akiongea mbele ya timu nzima ya wahabari wa Global.
Mwandishi: Baada ya uamuzi wa mahakama, mlichukua hatua gani?
Lissu: Hatukuwa na namna yoyote ya kuweka pingamizi mahakamani. Awali kama Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Chadema kwa niaba ya chama nilitoa waraka kwa watu wote waliotuhumiwa kukihujumu chama na ndiyo uliyosababisha kungo’lewa nyadhifa zao Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Dokta Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Mwandishi: Vipi kuhusu vyeo vyake vya kibunge baada ya chama chenu kumuona Zitto hafai?
Lissu: Mimi ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuna sheria nyingi Bungeni ambazo zitaeleza hatima ya Zitto kukaa sehemu ya kambi rasmi ya upinzani na wadhifa wake, hayo yataeleweka huko Dodoma.
Mwandishi: Kwani mashitaka yao mbele ya Kamati Kuu yalikuwa mazito kiasi gani?
Lissu: Dokta Mkumbo, Zitto na Mwigamba mashtaka yao na kashfa zilizokuwa zinawakabili ni nzito na wasingeweza kupona ndani ya Chadema. Ikumbukwe kuwa tuna vijana maridadi sana kwenye kitengo cha mawasiliano, mkakati wa Zitto na wenzake ulilenga kukimaliza chama chetu, tunamshukuru Mungu kugundua mapema.
Mwandishi: Unaweza kuyafafanua makosa yao?
Lissu: Nisingependa kurudia kuyabainisha makosa yao lakini napenda kusema kuwa Zitto atabakia kuwa mbunge wa mahakama, katika mkutano wangu na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jumanne Novemba 26, mwaka jana nilisema mengi kuhusu hilo.
Nilielezea jinsi wajumbe wote wa Kamati Kuu walivyofikia uamuzi wa kuwavua nyadhifa zao pale Blue Pearl Hoteli, Ubungo Plaza Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam, baada ya mjadala wa siku mbili na tukajadili masuala mbalimbali yakiwemo yale ya kutekeleza mikakati ya kichama kama vile operesheni za chama kama vile Oparesheni ya M4C (Movement for Change) nakadhalika.
Lissu akiongea na Mkurugnezi wa Global Publishers, Eric Shigongo.
Mwandishi: Unadhani watuhumiwa hao walitendewa haki na chama chenu?
Lissu: Watuhumiwa walitendewa haki kwa mujibu wa katiba yetu ya chama, walikabidhiwa mashitaka yao 11 kimaandishi na walitakiwa kuyajibu kimaandishi pia ndani ya siku 14 kuanzia tarehe waliyokabidhiwa. Baada ya kuwasilisha majibu ya tuhuma zao waliitwa kujieleza au kujitetea kwa nini wasinyang’anywe kadi za uanachama, hivyo waliofukuzwa, hawakuonewa kabisa.
Mwandishi: Kwa kuwa mkutano huo ulikuwa ni kwa ajili ya wajumbe wa kamati kuu ya chama, wananchi wakisema mliwaonea watuhumiwa kwa kuwa kilikuwa kikao cha siri, utasemaje?
Lissu: Katika mkutano ule haukuwa wa siri walihudhuria Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika, Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Rwakatare, Mkurugenzi wa Uchaguzi, John Mrema, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na viongozi wengine wa juu ndani ya Chadema.
Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:
Post a Comment