Siku moja baada ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kutangaza matokeo ya kidato cha nne na kuonyesha ufaulu kuongezeka kwa asilimia 15, wadau wa elimu wamepinga matokeo hayo kwa madai kuwa ubora wa elimu haukuangaliwa.
Hatua hiyo inatokana na mabadiliko ya viwango
vipya vya alama za ufaulu yaliyofanyika Oktoba mwaka jana, baada ya
Serikali kuweka alama za kufaulu zisizobadilika katika daraja A mpaka F
iliyotambuliwa kama kufaulu kusioridhisha.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),
Bashiru Ali alisema licha ya kiwango cha ufaulu kuongezeka, hakuna ubora
wa elimu uliozingatiwa. Dk Ali alisema kinachochangia hali hiyo ni
kuwapo kwa mfumo wa elimu wa kibaguzi, unaosababisha ubora wa elimu
unashuka, kwa kuwa badala ya kupimwa kwa ujuzi na maarifa hupimwa kwa
madaraja.
Dk Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu
cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Duce), alisema tatizo lililopo ni
mfumo mbaya wa ufundishaji, badala ya kuwekeza nguvu kukuza taaluma,
nguvu nyingi zimewekezwa kupanga madaraja.
Alisema matokeo hayo ni mazuri kwa Serikali, kutokana na kuzongwa na matokeo mabaya ya mwaka jana, lakini kitaaluma siyo mazuri.
0 comments:
Post a Comment