Mwalimu wa madrasa ya Ali Munawar, ustaadhi Mohamed Ngulanjwa (36)
wa Mbagala Mianzini jijini Dar es Salaam, ameuawa baada ya kumchinja
mwanafunzi wake.
Ustaadhi huyo aliyekuwa mwalimu wa madrasa na shule ya awali ya Ali
Munawar, alimchinja mwanafunzi huyo jana saa 12.10 jioni kwenye eneo
la madrasa baada ya kutenganisha kichwa na kiwiliwili
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Jonathan Shana, akizungumzia
mauaji hayo , alisema tukio hilo la kinyama, lilishuhudiwa na wananchi
waliomuua ustadhi huyo.
Alisema baada ya mwalimu kumuua mwanafunzi wake wa kiume alichukua kisu alichotumia pamoja na msahafu na kukimbia.
“Ilidaiwa kuwa alimchukua mtoto huyo , kumlaza chini kisha kumchinja
kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kutelekeza vipande vya mwili
wake kwenye varanda,” alisema Kamanda Shana.
Baada ya mauaji hayo mtuhumiwa alianza kukimbia lakini wananchi
walimvamia na kumshambulia kwa mawe na kila silaha iliyokuwa karibu na
kumuua papo hapo.
Shana alieleza kuwa polisi walifika eneo la tukio na kuchukua maiti hizo na kuzipeleka hospitali ya Temeke.
Hata hivyo alisema jina la mtoto huyo mwenye umri kati ya miaka 10- 12 halikufahamika na polisi inaendelea na uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment