Ray C ni Miongoni mwa mastar wa Bongo ambao waliingia kwenye matumizi
ya dawa za kulevya ingawa baadae alikuja kuacha baada ya kuanza kutumia
dozi rasmi ya kuacha matumizi ya dawa hizo.
Habari njema kutoka kwake kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa
taarifa kuhusu kufungua asasi ya kuwaelimisha vijana na jamii kuhusu
madhara ya utumiaji wa dawa hizo za kulevya.
Huu ni ujumbe wake:
Namnukuu:
"Ray C Foundation ni asasi ilioanza rasmi Feb 2014,nia na madhumuni ya hii asasi ni kuelimisha vijana na jamii yote kwa ujumla madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya kwani madawa ya kulevya ni tatizo kubwa sana lililoikumba nchi yetu ya Tanzania.
"Palikuwepo na ukimya mkubwa juu ya haya madawa ya
kulevya,majadiliano juu ya ulevi huu yalikuwa hayazungumziki kwa uwazi
hata kidogo japo madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ni makubwa sana
na yanatisha katika jamii yetu hapa Tanzania…….
"Nia na madhumuni ya kuaznisha Ray C Foundation hasa ni kuhamasisha na kueleimisha vijana nan jamii nzima athari za utumiaji madawa ya kulevya na kuwafikia walengwa ndani ya jamii na katika maeneo yao nchi nzima!!!
Eeh Mungu tuepushe na janga hili Nguvu kazi ya Taifa isipotee……… We need your Support……………"

0 comments:
Post a Comment