Kwa kipindi kirefu mkali wa ‘Single Boy’ Ali Kiba amekuwa kimya bila kutoa kazi yake binafsi huku ukimya wake ukizua maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa muziki Tanzania.
Lakini February 25 Ali Kiba amezua maswali mengine kwa
mashabiki wake baada ya kuweka kwenye Instagram picha inayomuonesha
akiwa na AY na Mwana Fa na kuandika ‘@Aytanzania&007#mj record #wait
for it bonge ya wimbo.’
Hata hivyo hakuweka wazi kama ni wimbo wake au ameshirikishwa na maswaiba hao.
Mtandao wa TimesFm imefanya mahojiano na Ali Kiba ambaye ameyajibu
maswali hayo yote, maswali ambayo hapo awali yalikuwa na majibu ya
kuhisia tu bila kuwa na uhakika.
Ali Kiba ameiambia TimesFm kuwa aliweka picha hiyo kwenye Instagram lakini hakuweka maelezo ya kutosha kwa makusudi.
“Sababu ya kuweka vile ni katika kutaka tu kuwa-surprise watu kwa
sababu sikupenda kuwambia ni ngoma ya nani ila nimewajulisha kuwa
nimefanya nao na tumefanya kwa MJ, hiyo yote ni kutaka kuwa-surprise.”
Amesema Ali Kiba.
Mwimbaji huyo amedai kuwa hadi sasa wimbo huo haujajulikana ni wa
nani kati yake yeye, Mwana Fa na AY, “tumefanya wote…haijajulikana ngoma
ni ya nani.”
Ali Kiba ameongeza kuwa mashabiki wampe miezi miwili ijayo na kisha
watapata maelezo ya kutosha kutoka kwake na kwamba baada ya muda huo
kila kitu kitakuwa sawa.
Mwimbaji huyo wa ‘My Everything’ ameeleza pia sababu za yeye kuwa
kimya, pamoja na mpango wake kwa mwaka 2014 ambapo amedai kuwa ataachia
albam yake mpya.
“Sababu ya kuwa kimya ni kumpush Abdu Kiba aweze kuwa sawa sawa na
vilevile mimi ni mzazi kwa hiyo niko busy na jinsi ya kuwa baba. Yaani
vitu vingi vyote nilikuwa nikifanya, wakati muda wote niliokuwa
nikifanya hivyo vitu nilikuwa najiandaa na albam yangu nyingine ambayo
ni ujio mpya…nakuja na everything.
“Albam ipo kwa sababu itakuwa chini ya usimamizi wa kampuni ambayo
inanihost, na ndio maana nikakwambia nipe miezi miwili na watu watajua
kila kitu kinachoendelea…itafanyika na usimamizi mzuri tu na process
zote zitakuwa ziko okay. Ila siwezi kukwambia ntafanya na distributor
gani lakini, wasimamizi wangu watafanya hilo, wasimamizi ambao
wamenichukua ndio maana ukaona kimya kingi, ni ku-fight maandalizi na
kumaliza ngoma.”
Sikiliza interview yote hapa:
>>Times 100.5 fm

0 comments:
Post a Comment