MTOTO WA BELINA ‘AOGESHWA MAHELA’



Mtoto wa mwanamitindo Belina Mgeni, Nayla Farid  ambaye amefanyiwa maulidi ya kutimiza siku arobaini juzikati, alijikuta akiloa minoti baada kila aliyetaka kumshika kumpa ‘nyekundu nyekundu’ na wengine Dola za Kimarekani.


Shughuli hiyo ilifanyika nyumbani kwa Belina, Mbezi Makonde jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali ambao mbali na kunywa na kula pia walionesha upendo wao kwa kumwaga zawadi lakini wengine walionesha makeke kwenye kutunza pesa.

Akizungumzia tukio hilo, rafiki wa karibu wa Belina  aitwaye Halima alisema: “Imefana, tunashukuru lakini kwa jinsi huyu mtoto alivyotunzwa pesa inaonekana atakuwa mtu wa kushika pesa sana ukubwani.”

Maulidi ya mtoto huyo yalipambwa na wanachuo waliosoma Kurani na kuimba  Kaswida tofauti na ambavyo imezoeleka kwa baadhi ya mastaa.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini