Luteni Kalama na Isabela Mpanda.
WALE wapenzi wa muda mrefu, Luteni Kalama na Isabela Mpanda hivi
karibuni walizinguana kinomanoma baada ya Kalama kwenda kumchomoa kwa
nguvu mpenzi wake huyo akiwa bandari ya Dar es Salaam alikokuwa akifanya
taratibu za kwenda Zanzibar kushuti filamu. Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio kilisema: “Sisi tulishangaa kumuona Kalama anakuja akiwa amefura, alipomuona tu Isabela akamchukua kwa nguvu, walizinguana sana na baadaye wakaondoka pamoja, hatukujua tatizo nini ila inaonekana kuna kitu.”
Isabela Mpanda.
Baada ya kuipata ishu hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Isabela na
alipopatikana alisema: “Kweli nilikuwa naenda Zanzibar lakini mbaya ni
kwamba sikumuaga, alipopata taarifa kuwa niko bandarini akaja
kunichomoa, lilikuwa ni tukio la aibu sana.”
Luteni Kalama.
Kwa upande wake Kala alifunguka kuwa, alifikia uamuzi wa kwenda
kumrudisha baada ya kusikia anaenda kushuti filamu Zanzibar bila
kumtaarifu hivyo akaona huko ni kuchezewa sharubu.
0 comments:
Post a Comment