HAYA NI MAJINA YA WASICHANA 10 BORA NA WAVULANA 10 BORA KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013

 
Watahiniwa wa kike wamefanya vizuri kwa kuchukua nafasi saba kati ya 10 za juu, huku Shule ya Marian Girls ya Pwani ikiongoza kwa kuwa na wanafunzi wanne.
 
Mwanafunzi aliyeongoza ni Robina Nicholaus wa Shule ya Marian Girls, akifuatiwa na Magrath Kakoko wa St Francis (Mbeya) wakati wa tatu ni Joyceline Marealle kutoka Shule ya Canossa (Dar es Salaam).
 
Wengine ni Safarina Mariki na Abby Sembuche wa Marian Girls, wakati wavulana pekee kwenye wanafunzi 10 bora ni Sunday Mrutu kutoka Anne Marie (Dar es Salaam) na Nelson Rugola Anthony na Emmanuel Mihuba Gregory wa Kaizirege (Kagera).
 
Wanaofuata ni Janeth Urassa kutoka Marian Girls (Pwani) na Angle Ngulumbi wa St Francis (Mbeya).
 
Wasichana 10 bora
Wasichana waliofanya vizur kwenye mtihani huo wameongozwa na Robina Nicholaus (Marian Girls), Magrath Kakoko (St Francis), Joyceline Leonard Marealle (Canossa), Safarina W Mariki, Abby T Sembuche na Janeth Urassa (Marian Girls).
 
Wengine ni Angle Ngulumbi (St Francis), Getrude James Mande wa Precious Blood (Arusha), Violet Mwasenga wa St Francis na Catherine Swai kutoka Marian Girls.
 
Wavulana 10 Bora
Wavulana waliofanya Vizuri ni Sunday Mrutu wa Anne Marie, Nelson Rugola Anthony na Emanuel Mihuba Gregory wote kutoka Kaizirege, Razack Hassan wa St Matthew’s (Pwani) na Hamis Msangi kutoka Eangles (Pwani).
 
Wengine ni Joshua Zumba wa Uwata (Mbeya), Brian Laurent na Mohamed Ally wa Marian Boys (Pwani), Shahzill Msuya wa St Amedeus (Kilimanjaro) na Shabani Hamisi Maatu wa Mivumon Islamic Seminary (Dar es Salaam).
 
Shule za serikali hoi
Matokeo yanaonyesha kuwa shule kumi za kwanza ni za binafsi tu na shule za Serikali zimeanguka vibaya.
 
Shule bora ni St. Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Girls ya Dar es Salaam, Precious Blood ya Arusha, Canossa ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Anwarite Girls ya Kilimanjaro, Abbey ya Mtwara, Rosmin ya Tanga na Don Bosco Seminary ya Iringa.
 
Katika shule zenye watahiniwa chini ya 40 shule iliyoongoza ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, Thomas More Machrina ya Dar es Salaam, Mwanza Alliance ya Mwanza na Queen of Apostles Ushirombo Seminary ya Geita. 

Nyingine ni St Joseph Kilocha Seminary ya Njombe, Bethelsabs Girls ya Iringa, St Mary Junior Seminary ya Pwani, Maua Seminary ya Kilimanjaro na Hellen’s ya Dar es Salaam.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini