LOWASSA AANGUSHA BONGE LA PATI NYUMBANI KWAKE


WAZIRI  Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Ngoyai Lowassa ameangusha bonge la pati la kuukaribisha mwaka 2014.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akizungumza katika sherehe ya mwaka mpya nyumbani kwake Ngarashi Monduli.Pembeni yake ni mkewe mama Regina Lowassa.
Tukio hilo lililojaa furaha ya aina yake lilifanyika Januari 1, mwaka huu nyumbani kwake Ngarashi- Monduli, mkoani hapa ambapo mamia ya watu walijumuika pamoja na mbunge huyo kuukaribisha mwaka.
Lowassa aliyeonekana na sura ya furaha, alishika kifaa chenye mkia wa ng’ombe ambacho ni cha asili na kuwasalimia waalikwa kwa kukichezesha kuashiria sherehe imeanza na watu waukaribishe mwaka mpya.
Mbali na wageni waalikwa, Lowasa alijumuika na familia yake akiwemo mkewe, Regina Lowassa ambaye pia alionekana akiambatana na mumewe kwa kuwasalimia ndugu wageni waalikwa.
Katika pati hiyo ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya, watu walikunywa, walikula hadi kusaza.
Waalikwa walimuomba Mh Lowassa kujenga utaratibu huo kila mwaka, ili kudumisha umoja na mshikamano.                     

Waalikwa katika shughuli hiyo, walikuwa ni pamoja na maaskofu na viongozi wengine wa dini wa ndani na nje ya nchi.
Waalikwa hao walimpongeza Mh Lowassa kwa kitendo cha kuamua kujumuika pamoja na ndugu zake na viongozi mbalimbali kwani kimeonesha ishara ya upendo.
“Ni jambo zuri sana Mh Lowassa amefanya kwa ndugu zake. Mwaka mpya ndiyo huu unaanza hivyo si vibaya akikutana na kufurahi pamoja na wadau mbalimbali,” alisema mmoja wa waalikwa.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini