KIBANDA: MAGUFULI ANASIFIWA TANZANIA WAKATI HANA LOLOTE

Absalom Kibanda: Magufuli anasifiwa Tanzania wakati hana lolote
Akiwa katika kipindi cha TV cha Asubuhi Leo ya Channel Ten, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw. Absalom Kibanda amesema Magufuli anasifika sana Tanzania kwa kujenga barabara kwa sababu watu hawajatoka nje ya nchi na kuona wenzetu wanavyojenga barabara. Akasema utamsifiaje Magufuli wakati foleni imejaa na inatisha? Akasema ni watu kuwa na fikra finyu na kutokujua kinachoendelea duniani. 
Hii inanikumbusha maneno ya rafiki yangu mmoja anayefanya kazi Ivory Coast ambaye pia aliwahi kuniuliza hivi Tanzania wanamsifia kwa kujenga barabara zipi? Watu hawajaona wenzetu wanavyojenga barabara. Siyo unatumia trilioni kuikarabati Mandela road kwa lanes mbili zilezile na foleni ikabaki pale pale! Kinachomsaidia Magufuli ni ubabe tu but he is empty!

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini