MKUU wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe, amekerwa na tabia ya watendaji wengi wa serikali kutowajibika ipasavyo na matokeo yake kuwabebesha mizigo mawaziri na Rais.
Alisema chanzo cha wizara nyingi kutofanya vizuri kunasababishwa na
mfumo mbaya ulioendekezwa na baadhi ya wakurugenzi,makamishna, makatibu
na watendaji walioko chini yao kukosa uzalendo wa kuwajibika kwa
wananchi.
Akitoa hutuba fupi jana katika mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha
Akiba na Mikopo cha Bunda (Bunda SACCOS), alisema wananchi wako tayari
kuwajibika isipokuwa kikwazo ni baaadhi ya watendaji hao wa serikali
kuwa miungu watu.
Aliongeza kuwa sheria ya utumishi ya kuwachukulia hatua za kisheria
watendaji wasiowajibika ina mlolongo mrefu jambo linalokwamisha
uwajibikaji, hivyo alishauri sheria hizo zirekebishwe.
Mirumbe alisema shughuli nyingi za Serikali hukwamishwa na watumishi
wa kati ngazi za halmashauri, mikoa na kwenye wizara huku wakijua kuwa
mishahara yao ni kodi ya wananchi wanaonyanyaswa.
Alikuwa akijibu taarifa ya Mwenyekiti wa SACCOS hiyo, John
Kitang’osa, aliyesema kuwa yapo maombi mengi ambayo wamepeleka kwa
Serikali kupitia taasisi zake, lakini majibu hayatolewi kwa wakati
muafaka.
0 comments:
Post a Comment