Hemed na Mlela wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya kuumizana huku mama yao akiwaangalia kwa huzuni
Kasha la filamu mpya ya bifu la kina Mlela na PHD inayotarajiwa kuingia mtaani keshokutwa Jumatano.
LILE bifu lililowahi kufukuta kwa kasi
mithiri ya moto wa kifuu baina ya ‘tozi’ wawili ndani ya tasnia ya
filamu, Hemed Suleiman ‘PhD’ na Yusuf Godfrey Willard Mlela ‘Mlela’
linadaiwa kuibuka upya na kuzidisha uhasama baina ya wasanii hao. Aidha,
alisema bifu hilo lilidhihirika hivi karibuni wakati wawili hao
walipokutanishwa kuigiza filamu moja, kwani mara kwa mara walijikuta
wakifanya kweli kwenye baadhi ya vipande vya ugomvi na mapigano jambo
lililompa wakati mgumu muongozaji wa filamu hiyo inayotarajiwa kuingia
sokoni kuanzia Desemba 18 mwaka huu iliyopewa jina la I Know You.
“Walikuwa na muda mrefu sana bila
kukutana, tukadhani bifu lao halipo tena, lakini hivi karibuni
walikutana kwenye filamu iliyoandaliwa na Mtitu Game 1st Quality, wakawa
wanafanya kweli kwenye baadhi ya sehemu za majibizano na mapigano huku
wakifanyiana fujo mbalimbali huku kupigana vijembe vya wazi,” alisema
rafiki huyo.
“Ni kweli tulikuwa na utofauti, ule
mvutano wa zamani bado ulikuwepo, kila mmoja hakutaka kuwa dhaifu kwa
mwenzake, utaona baadhi ya vipande tulivyofanya kweli,” alisema Mlela
ambapo simu ya Hemed iliita bila kupokelewa licha ya mwandishi wetu
kuipiga mara kwa mara.
Naye Meneja matayarishi wa Kampuni ya Game
st Quality Ltd, Noel Amani ‘Futo’ alisema filamu ya I know You iliwapa
wakati mgumu sana kutokana na bifu la wasanii hao kuonekana waziwazi.
“Walitumbua sana, kuna wakati walifokeana
kweli, kukunjiana ngumi hata hivyo kuna baadhi ya vipande walivyofanya
kweli tumelazimika kuviacha ili kuleta uhalisia zaidi. Kila mmoja
anaamini yuko juu ya mwenzake,” alisema Futo.