

Tivoli Athuman, mkazi wa Mwenge jijini Dar, alisema ni bora Rais
akalivunja bunge hilo kwa vile wajumbe wake wameonyesha udhaifu mkubwa
wa kushindwa kutetea hoja zenye masilahi kwa wananchi, badala yake
wameweka mbele utashi wao binafsi na vyama vyao.

“Wote tunajua kwamba kinachotafutwa pale ni katiba ya wananchi wote
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ni jambo la ajabu kuona
wajumbe wanafika pale na kutanguliza misimamo yao na vyama vyao
utafikiri ndicho walichotumwa na wananchi, mimi nafikiri JK
angelivunjilia mbali bunge hili,” alisema.

“Hakukuwa na sababu ya kuwajumuisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
tumeshawaona hawa ni watu wa malumbano tokea mwanzo, kuwaleta huku ni
kuvuruga mambo tu, hapa ilibidi Rais ateue mwenyewe wajumbe wasio
wanasiasa.
0 comments:
Post a Comment