Baada ya kutolewa video yake ya Nimevurugwa kwenye tuzo za KTMA 2013/2014, Snura amefunguka kuhusu kile ambacho kilionekana kusababisha video yake kufungiwa na kutolewa kwenye mashindao ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards kwa kudai kuwa kiuno chake ndo tatizo hivyo katika video yake mpya hakutakuwa na mauno ya mitego!:
"Snura mpya ataonekana kwenye video ya Ushaharibu na
itapendwa sana video hiyo.Nimekatika kidogo ila hakuna mauno kama kwenye
Nimevurugwa." Amesema Snura
Pia Snura kaomba radhi kwa Mashabiki watakaokosa mauno yake kwenye
video zijazo na kusema atakayetaka kuona mauno hayo atayakuta kwenye
show anazofanya.

0 comments:
Post a Comment