Mkongwe kwenye sanaa ya uigizaji Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’.
MKONGWE kwenye sanaa ya uigizaji Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’
amefunika mbaya katika uchezaji wa muziki ambapo aliwatoa jasho hadi
vijana wadogo.
Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilinaswa na paparazi wetu,
wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya bethdei ya Klabu ya Bongo Movie
Unity, iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Arcade,
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
“Ha! Kweli nimeamini mjini hakuna mzee, uzee mwisho Chalinze, mjini
kila mtu baby. Hebu ona Bi. Mwenda anavyocheza vizuri. Yaani anawafunika
hadi vijana wadogo kabisa. Ni burudani sana jamani.
“Tazama alivyopendeza, amepangilia rangi za nguo vizuri. Kweli leo
ni siku ya furaha, ndiyo maana ameamua kutoka tofauti na siku
nyingine,” mmoja wa wasanii alisikika akiwaambia wenzake ambao
walimuunga mkono.
0 comments:
Post a Comment