
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa,
atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo
ambao hawathamini mastaa.

“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na
hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama
wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.

“Unajua Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni
lakini wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa
sababu ya kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa
kabisa, mimi siwezi kuolewa na Mbongo.”
0 comments:
Post a Comment