Mimi FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la
CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi
mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza
sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.
Ndugu
MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba
kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo
vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
Ndugu
MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na
kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea
huyu hajui
kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na
amepoteza sifa za kuwa mgombea.
Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za
wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa
mgombea. Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na
hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio
muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya
kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini
28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la
CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni:
JINA LA MDHAMINI NAMBA YA KADI KURA
1. HABIBU ALLY SAIDI *16886275*
2. MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
3. ABDULKADIR ALLY *49264905*
4. SHABANI SULEYMAN *16984045*
5. JUMA MRISHO *48759563*
6. RAJABU ALLY *16872368*
7. MANENO MIRAJI *16872059*
1. HABIBU ALLY SAIDI *16886275*
2. MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
3. ABDULKADIR ALLY *49264905*
4. SHABANI SULEYMAN *16984045*
5. JUMA MRISHO *48759563*
6. RAJABU ALLY *16872368*
7. MANENO MIRAJI *16872059*
Wananchi wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini
kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura
kwenye maeneo ambayo wamejazwa wanatokea.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki
ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini.
Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY amedanganya Uraia wake, na kwamba yeye si
Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia
wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.
Hivyo ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ndugu MATHAYO.M.TORONGEY kwa kuwa
anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.
Wako katika ujenzi wa Taifa
FABIAN LEONARD SKAUKI
……………………………………………………..
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.
THE CIVIC UNITED FRONT
0 comments:
Post a Comment