SHILOLE: SIKUMPA BARNABA MAPENZI YANGU


Shilole akifanya mahojiano na Global TV Online.
MAAJABU! Licha ya ulimwengu wa burudani Bongo kuamini kwamba staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliwahi kuanguka dhambini kwa Mbongo-Fleva, Elias Barnaba, mwanadashosti huyo ameibuka na kudai kuwa hakuwahi kumpa penzi.
 
Shilole anayetamba na Ngoma ya Nakomaa na Jiji, amefunguka hayo kupitia Global TV Online ambapo mahojiano hayo yatarushwa kwenye Mtandao wa Global leo, Jumatatu.
“Ukweli sikumpa penzi Barnaba, yule ni mshkaji tu…kama ni muziki hakunipiga tafu kama alivyonisaidia Q-Chillah …hahaha acha hizo bwana, Barnaba hakuwa mchumba wangu,” alisema Shilole.
Elias Barnaba.
Mbali na kumfungukia Barnaba kwenye kipindi hicho, Shilole amefunguka mambo mengi ambayo hajawahi kuyasema, hivyo ukitaka kupata uhondo zaidi, tembelea Mtandao wa www.globalpublishers.info utapata kuiona Global TV Online.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini