STAA wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa jukwaani akifanya shoo ya kidunia na kupewa darasa la wokovu.

Zuwena Mohamed ‘Shilole’(kulia) na Mchungaji.
Tukio
hilo lililowagusa wengi, lilitokea juzikati katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee, jijini Dar ambapo mchungaji huyo ambaye hakupenda
kujitambulisha jina lake, alifuatilia shoo ya Shilole kisha akamwita
kumpa darasa la wokovu.

Akizungumzia
tukio hilo kwa kinasa sauti cha Weekly Exlusive Star, Shilole aliweka
plain kuwa, mchungaji huyo aliguswa na namna ambavyo watu wengi walikuwa
wakifuatilia shoo yake, akaona anaweza kuwabadilisha wengi waliopotea
kupitia wokovu.
“Aisee ilikuwa noma, nilipoona ananiita nilishtuka kidogo. Mbaya zaidi aliniambia anataka tupige picha pamoja, ndipo alipoanza kunipa darasa la wokovu.
“Alinitaka
nibadilike kimavazi, pia nisimsahau Mungu katika maisha yangu yote na
alimalizia kwa kunitaka niende kanisani kwake ili ikwezekana nitumie
uimbaji wangu kuwabadilisha wengi waweze kumtumaini Bwana,” alisema
Shilole staa wa wimbo Nakomaa na Jiji.
Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, Shilole alionekana kuguswa na maneno ya mchungaji huyo na kusema yamemkumbusha suala la kumkumbuka Mungu kila wakati katika kazi za mikono yake.
Akasema kwa kuzingatia hilo, sehemu ya mapato yake atakuwa akiyatumia katika kutoa sadaka husan kwa watu wasiojiweza ili kutimiza amri ya Mungu. “Ni wakati wa kubadilika, huu muziki tunafanya upo na utaendelea kuwepo lakini jambo la muhimu sana ni kumuabudu Mungu katika siku zote za maisha yetu ya hapa duniani,” alisema Shilole.
“Aisee ilikuwa noma, nilipoona ananiita nilishtuka kidogo. Mbaya zaidi aliniambia anataka tupige picha pamoja, ndipo alipoanza kunipa darasa la wokovu.

Hata hivyo, katika mazungumzo hayo, Shilole alionekana kuguswa na maneno ya mchungaji huyo na kusema yamemkumbusha suala la kumkumbuka Mungu kila wakati katika kazi za mikono yake.
Akasema kwa kuzingatia hilo, sehemu ya mapato yake atakuwa akiyatumia katika kutoa sadaka husan kwa watu wasiojiweza ili kutimiza amri ya Mungu. “Ni wakati wa kubadilika, huu muziki tunafanya upo na utaendelea kuwepo lakini jambo la muhimu sana ni kumuabudu Mungu katika siku zote za maisha yetu ya hapa duniani,” alisema Shilole.
0 comments:
Post a Comment