
Mastaa wawili, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Rose Ndauka wamedaiwa kuwa kwenye bifu chanzo kikidaiwa ni Rose kumtibulia mwenzake dili la ile project ya kusafisha jiji iliyofanyika hivi karibuni.

Akizungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotajwa jina lake, chanzo
kilisema, wazo la project ile alikuwa nalo Batuli lakini Rose akaingilia
kati, hali iliyosababisha Batuli amnunie mwenzake.

Alipopigiwa Batuli kwanza aling’aka lakini akasema hapendi
kuzungumzia mambo hayo kwani yameshapita huku Rose akieleza kuwa, wazo
la project hiyo alikuwa nalo kabla hajajifungua hivyo haoni kama
kamtibulia Batuli dili lake.
0 comments:
Post a Comment