RAIS JAKAYA KIKWETE ALIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO MKOANI DODOMA

Nawapongezeni kwa Kuwa sehemu ya Kuandika historia Mpya kwa Taifa la Tanzania,Mkitunga Katiba Bora Majina yenu yataandikwa kwa Wino wa Dhahabu.
 
Naombeni Mtunge Katiba Itakayo Dumisha Umoja wetu,Asili zetu,Katiba ambayo haitatutenganisha kirangi,Kisiasa au Kiimani. 
 
 Kihistoria hii ni Mara ya 3 Katiba ya Tanzania Inatungwa Upya,Tofauti na Vipindi Vingine.Kipindi hiki Utungaji wa Katiba Umeshirikisha Wananchi wengi zaidi. 
 
Msukumo Mkubwa sana wa Kudai Katiba Mpya Ulianza baada ya Mfumo wa Vyama Vingi,Wengi walizani kuwa Kudai  Katiba Mpya kutawasaidia Kushinda chaguzi dhidi ya CCM.La hasha!!! 
 
Desemba Mwaka 2012 nilitangaza Kuanza Mchakato wa Kutunga Katiba Mpya,Kazi hii ilipewa Tume ya Kukusanya Maoni ya Watanzania..
 
Mchakato Mzima wa Katiba Utahitimishwa na Wananachi kwa Kuipigia Kura ya Maoni kama wanaikubali Katiba au La!!! 
 
Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume Kuwasilisha Rasimu ya Katiba Mpya Tar.18/03/2014 hapa Bungeni,Ilikuwa ndio Mwisho wa Kazi ya Tume ya Warioba, kazi iliyobakia ni Kwenu Wabunge. 
 
Naishukuru sana Tume ya Warioba Rasimu walioitunga inaleta Mambo mengi kwenye Katiba Mpya ya Tanzania,Ni Rasimu Nzuri. Rasimu inamambo mengi sana .
 
Naombeni sana Msome Rasimu ya Katiba Yote kwa Makini,Sio unafundishwa cha Kusema,Unafundishwa Uzungumze nini.Akili za Kuambiwa Chnganya naza kwako.
 
Kama Kuna Jambo halifai kwenye Rasimu Wajumbe Msisite kulifuta.
 
Tungeni Katiba ambayo Watanzania wataipenda,Sio Mtunge katiba baada ya Muda Mfupi manataka kurekebisha,Msitunge Katiba Mpya isiyoweza Kutekelezeka.
 
Rais  Kikwete amesema ‬ Kuna sehemu Rasimu Inamapungufu sana.,Ibara ya Pili inaacha Maziwa na Mito kuwa ni Sehemu ya Tanzania.
 
MUUNDO WA SERIKALI TATU.
Kuna Mambo yanayopendekezwa na Tume Mf.Viwanda,Afya n.k yapo kwenye Serikali ya Nchi za Ushirika.
  
Serikali ya Muungano inahusisha,Katiba,Usalama (Baadae bado)  Mambo mengi yanatekelezeka Kupitia Serikali ya Muungano tuliyo nayo sasa,Rasimu ya Serikali tatu inawaweka wapi watumishi?Naomba Msome sana Rasimu yote. 

Rais amesema Ibara ya 128 inayoleta dhana ya Kupoteza Ubunge kutokana na Kutofanya kazi za Kibunge kwa Tatizo la Maradhi au kizuzini kwa Muda wa Miezi 6.Someni kwa Makini kipendele hiki,Jambo hili liwekwe Vizuri.
  
Yaani Mbunge augue Miezi sita Mfululizo eti afukuzwe,Huu ni Ukatili Usiotakiwa kwenye Katiba Mpya.
 
Pia kuhusu Mbunge kuwa Bungeni kwa Vipindi Vitatu,Sasa Kama Mtu ameingia akiwa na Miaka 25 anamaliza akiwa na Miaka 40.Hii si sawa,Ni kunyimana Fursa.Hatuwezi Kupata Viongozi wa Kutengenezwa kwa Namna hii,Viongozi watatoka wapi wakati kila anapofikia hatua ya Kukomaa Ukomo wake umefika.

MUUNDO WA SERIKALI.
Hii ndio Ajenda Mama,Ombi langu Kwenu Kwanza Muwe watulivu mnapojadili Swala hili,Mkilijadili kwa Jazba wenye hasira hawa Jengi,Wenye hasira hawatengenezi jambo Vizuri.Uamuzi usio kuwa sahihi kwenye Jambo hili Unahasara Kubwa,Tanzania inaweza kuwa Nchi iliyojaa Migogoro yenye Matatizo ambayo hatujawahi kuwa nayo.

Kudai Serikali tatu sio Jambo Jipya,Ulikuwepo wakati Wa Kuunganisha Nchi zetu Mbili,Wakaamua Serikali mbili.


Imependekezwa Mara Nyingi lakini Halikukubalika,Bora Mzungumze kama linakubaliwa likubaliwe,kama Linakataliwa Likataliwe.

Waasisi wa TAIFA LETU Waliamua Kuchagua Muundo wa Serikali Mbili.


1.Ni muundo Usio Imeza Zanzibar.
2.Tanganyika  kubeba  mzigo  wa  kuihudumia  Zanzibar.


Ni vigumu sana Kuacha Kujadili Figa za Wazee wetu hawa,Wao ndio Wakwanza kutuletea Mfumo huu.

Zungumzeni hoja zao,Zungumzeni muone hoja zao.
Mfanye Maamuzi "Informed Decision" .Wapeni Heshima ya Kujadili Mawazo yao,Yanani ni Bora kuliko ya hawa Wazeee??
 


Kwa  mujibu  wa  tume  ya  Warioba ,  
1. Serikali  tatu  ndo  matakwa  ya  watanzania  wengi
2.Serikali  tatu  zinatoa  majibu  ya  changamoto  za  sasa  za  muundo  wetu....

Rais  amesema  kuwa  wapo  wanaokubaliana  na  tume, lakini  pia  wapo  wanaopinga. 

Wanaopinga  wanasema  kuwa  takwimu  za  tume  ya  Warioba  hazionyeshi  wala  kuthibitisha  madai  ya  kwamba  watanzania  wengi  wanataka  serikali  tatu...

Rais  amedai  kuwa, Watu  351664  walijiandikisha  kutoa  maoni  ambapo  kati  yao, watu  47820, sawa  na  asilimia  13.6  ndio  waliodai  kukerwa  na  muundo  wa  muungano...

Asilimia  86.4   walidai  kuwa  hawana  tatizo  na  muundo  wa  muungano ...

Sasa, Iwaje  asilimia  13.6(  waliotoa  maoni )  igeuke  kuwa  ya  watanzania  wengi???

Kwa  takwimu  hizi, madai  ya  tume  kwamba  watanzania  wengi  wanataka  serkali  tatu  si  ya  kweli.....

Kuhusu  madai  ya  tume  kwamba  serikali  tatu  itatatua  changamoto  zinazoukabili  mfumo  wa  serikali  mbili, Rais  alianza  kwa  kutaja  faida  za  Serikali  mbili  na  changamoto  za  serikali  tatu:

Faida  za  Serikali  mbili:
1.Imesaidia  sana  kudumisha  amani
2.Inatoa  wepesi  wa  kusimamia  na  kuiongoza  serkali
3. Mkubwa  kutommeza  mdogo ( zanzibar )

Changamoto  za  Serikali  tatu:
1.Gharama  kubwa  za  uendeshaji  wa  shughuli  za  umma
2.Kuibuka  kwa  sera  kinzani
3. Namna  ya  uchangia  wa  gharama  za  serikali  ya  tatu ( ya  muungano )
4. Tofauti  za  kimaendeleo

Mlolongo  huu  unadhihirisha  kuwa  muundo  wa  serikali  tatu  hautapunguza  matatizo  na  badala  yake  utatuongezea  matatizo  zaidi

Rais  amekiri  uwepo  wa  changamoto  ndani  ya  muundo  wa  sasa  wa  serikali  mbili, lakini  akadai  kuwa changamoto  hizo  zinaweza  kupatiwa  ufumbuzi  pasipo  na  uwepo  wa  serikali  nyingine  ya  tatu!

Rais  Kikwete  amesema  kuwa  Serikali  ya  tatu  itakayoundwa  ni  serikali  ambayo  haina  chanzo  chochote  cha  mapato  cha  kuiwezesha  kujiendesha, hivyo  kuna  hatari  ya  shughuli  za  serikali  ya  muungano  kukwama  kwa  sababu  haina  nyenzo  yoyote  ya kuonesha  kwamba  mapato  yanawakilishwa....


Rais  alidai  kuwa, tume  ya  Warioba  ilipendekeza  kuwa, Serikali  hii  inaweza  kukopa  ili  iweze  kujiendesha...Amefafanua  kuwa, hii  ni  serikali  ambayo  haina  rasilimali  yoyote  zaidi  ya  jeshi, polisi  na  mahakama, hivyo  ni  serikali  ambayo  haikopesheki....

Rais  Kikwete  amesema  kuwa  Watanzania zaidi ya 90% wamezaliwa baada ya 1964! .Ikishatengenezwa Tanganyika, masharti yataibuka! Watu wataanza kuwa wageni... Watakaotoka upande wa pili wa Muungano

Ikishazaliwa Tanganyika, chuki za Utaifa zinaweza kuanza; na zitatufikisha pabaya! Rais  ameeleza kuwa,hata Tume ya Mabadiliko hawana majawabu ya uhakika juu ya kero zitakazotokana na serikali tatu!

"Kama mnaamua tuuvunje Muungano, vunjeni lakini si wakati nikiwepo"...Amesema Rais Kikwete

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini