Ashura Rashid ‘Saladini’.
NYUMBA ya msanii wa filamu za Kibongo aliyewahi kutamba na muvi kali
ya Saladini, Ashura Rashid ‘Saladini’ imeteketea kwa moto na kusababisha
hasara kubwa, huku msanii huyo akihaha kusaka hifadhi kwa majirani,
Chande Abdallah anakujuza.
Tukio
hilo lilitokea asubuhi ya Machi 6, mwaka huu maeneo ya Bugando jijini
Mwanza wakati msanii huyo akiwa kwa majirani zake ambapo chanzo cha moto
huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Akizungumza
na Showbiz kwa njia ya simu, Saladini alisema kuwa kwa sasa analala kwa
majirani kwa kuwa kila kitu chake kimeteketea kwa moto.
“Namshukuru
Mungu hakuna aliyedhurika lakini nimepata hasara kubwa sana kwani
hakuna kitu kilichotoka salama humo ndani,” alisema Saladini kwa
masikitiko
0 comments:
Post a Comment