Anaitwa Rajab Mwami Shamweshi.
Mambo hadharani! Kigogo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo anayewagombanisha mastaa wawili Bongo, Jacqueline Wolper Massawe
na Husna Maulid ni huyu hapa.
Habari zilizolifikia Ijumaa zilidai kwamba
baada ya mtafaruku wa mastaa hao kuripotiwa na gazeti mama la hili,
Uwazi la Jumanne iliyopita, jamaa huyo aliibuka na kuanza kulalamika kwa
watu wake wa karibu kuwa anachafuliwa mitandaoni kwa sababu ya mastaa
hao.

PATCHOU MWAMBA NDANI
Ilidaiwa kuwa Mwami alichukizwa na ishu hiyo kwani ilimhusisha mwanamuziki wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia ni mwigizaji, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ kuwa ndiye humkuwadia kwa mastaa.
Ilidaiwa kuwa Mwami alichukizwa na ishu hiyo kwani ilimhusisha mwanamuziki wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia ni mwigizaji, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ kuwa ndiye humkuwadia kwa mastaa.

Rajab Mwami Shamweshi Mkongo anaedaiwa kuwagombanisha Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid
TUANZE NA PATCHOU
Kabla ya kumpata Mwami mwenyewe, Ijumaa lilizungumza na Patchou uso kwa uso amba alifunguka anachokijua juu ya sakata la Wolper na Husna kumgombea mwanaume huyo.
Kabla ya kumpata Mwami mwenyewe, Ijumaa lilizungumza na Patchou uso kwa uso amba alifunguka anachokijua juu ya sakata la Wolper na Husna kumgombea mwanaume huyo.
Alisema: “Mimi nashangaa kuona nachafuliwa mitandaoni lakini ukweli anayefanya hivyo ni Husna.
“Huyo Husna ni kweli aliwahi kutoka na Mwami lakini baadaye alimdharau Mwami kwa sababu alimuona hana pesa.
“Huyo Husna ni kweli aliwahi kutoka na Mwami lakini baadaye alimdharau Mwami kwa sababu alimuona hana pesa.

“Baada ya kuona pesa zimemtembelea Mwami akataka kurudi ndipo akakuta
jamaa ameshajiweka kwa Wolper. Hapo ndipo Husna akaanza
kuchanganyikiwa.” Patchou aliendelea kuweka wazi kwamba yeye na Mwami ni
mtu na rafiki yake na pia ni ‘mapatna’ kwenye biashara.
Alisema amekuwa akikutana naye mara kwa mara Nairobi, Kenya na ndiye
aliyemleta Bongo kwa ajili ya kuanzisha kampuni ya michezo ambapo
alifikia hotelini.

Rajab Mwami Shamweshi.
KUWADI?
Alitiririka kwamba hajawahi kumkuwadia mwanamke lakini anachojua Mwami ni anajuana vizuri na
Wolper kwani alimtambulisha walipokutana Nairobi hivi karibuni ndipo akaujua uhusiano wao.
Alitiririka kwamba hajawahi kumkuwadia mwanamke lakini anachojua Mwami ni anajuana vizuri na
Wolper kwani alimtambulisha walipokutana Nairobi hivi karibuni ndipo akaujua uhusiano wao.
Patchou: “Nilishangaa kwa sababu baada ya Mwami kutua tu Bongo, wasichana wa mjini walipojua
ndipo wakaanza kumsaka hadi chumba alichofikia hotelini.“Wengine walidiriki hata kumtumia picha za utupu ili kuwa naye kimapenzi baada ya kupata namba yake.”
ndipo wakaanza kumsaka hadi chumba alichofikia hotelini.“Wengine walidiriki hata kumtumia picha za utupu ili kuwa naye kimapenzi baada ya kupata namba yake.”
Patchou alisisitiza kuwa yeye si kuwadi kama wanavyomtangaza kwani
hata huyo Wolper alishtukia amekutana naye Nairobi wakiwa na Mwami kwani
kabla ya hapo alikuwa hajuichochote.
Baada ya kumaliza kutoa utetezi wake, aliombwa kumpigia simu Mwami na kumuweka loud speaker
(sauti ya juu) ambapo alimweleza Mwami kila kitu ndipo akakubali kuzungumza na wanahabari wetu akiwa London, Uingereza.
(sauti ya juu) ambapo alimweleza Mwami kila kitu ndipo akakubali kuzungumza na wanahabari wetu akiwa London, Uingereza.
KIGOGO AFUNGUKA
Akizungumzia sakata hilo, Mwami ambaye anadaiwa kuwa na ‘mihela’ hivyo kujitwalia taito ya ukigogo alisema kuwa anamfahamu Husna kama mtu wa kawaida ambaye aliwahi kufahamiana naye.
Akizungumzia sakata hilo, Mwami ambaye anadaiwa kuwa na ‘mihela’ hivyo kujitwalia taito ya ukigogo alisema kuwa anamfahamu Husna kama mtu wa kawaida ambaye aliwahi kufahamiana naye.

Kwa upande wa Wolper alisema kuwa anamfahamu kwa kumsikia na kumuona lakini si kimapenzi kama wanavyomchafulia jina.
“Nilipokuja Tanzania kwa mara ya kwanza nilifikia
hotelini…(anaitaja), kama wanavyodai hata chumba ndicho chenyewe lakini
sikuja kwa ajili ya starehe za kimapenzi na wanawake, nilikuja kwa
biashara zangu, nashangaa kuona nawekwa mitandaoni hovyo na anayeniweka
namfahamu.
“Naomba nisizungumze sana, niishie hapo nikirudi Tanzania nitaongea nanyi kwa uwazi kabisa,” alisema Mwami.
Wolper na Husna ambao waliwahi kuwa mashosti walianza manenomaneno hivi karibuni ambapo awali haikujulikana chanzo hadi pale Husna alipoamua kulifungukia hilo la mwanaume.
Ijumaa lilifanya jitihada za kumsaka Wolper kupitia simu yake ya
mkononi, alipopatikana alisema angefika ofisini kwetu kutoa ufafanuzi
lakini mpaka gazeti linakwenda mtamboni alikuwa hajafika na alipotumiwa
sms ya kuulizwa kama angefika au la hakujibu.
0 comments:
Post a Comment