Hatimaye leo Bunge maalum la Katiba limemchagua Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wake mjini Dodoma.
Hii
inakuja baada ya jana kumchagua Mhe.Samweli Sitta kuwa Mwenyekiti. Mhe
Hassan alichaguliwa kwa kura 390 sawa na asilimia 74.6 na kumshinda
mpinzani wake Amina Abdalla Amour. Kura 7 ziliharibika - kama jana.
Katibu
wa Bunge hilo Maalum
ataapishwa na Rais Jakaya Kikwete kesho asubuhi Ikulu ndogo Dodoma.
Katibu
wa Bunge ndiye atakayemwapisha Mwenyekiti na Makamu wake, na Mwenyekiti
atawaapisha wajumbe wote, ndipo shughuli itapoanza rasmi ya kuandika
katiba mpya.

Mhe.Samia Suluhu Hassan (anaye angalia kamera)akipongezwa na aliyekuwa mshindani wake Mhe Amina Abdalla Amour mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa Bunge
la Maalum la Katiba mteule Dodoma, akishukuru wajumbe kwa kumchagua

Wajumbe
kinamama wakishangilia mara baada ya Bunge Maalum la Katiba kumpata
Makamu Mwenyekiti Mhe.Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma leo




0 comments:
Post a Comment