MAYASA: BADO SIJAONA MWANAUME WA KUZAA NAYE

Staa wa Bongo Muvi Mayasa Mrisho, alimaarufu 'Maya'.
Msanii mahiri wa filamu za hapa Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa katika pitapita zake zote bado hajaona mwanaume ambaye anaweza kuwa naye na kumzalia mtoto kwani wote anawaona ni waluwalu.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Maya alisema kuwa hakuna kitu anachokitamani kama kupata mtoto lakini kila akifikiria mtu anayeweza kupata naye mtoto ndipo ugumu unapokuja.
“Yaani mimi kama mtoto napenda sana kuwa naye lakini kinachonikera zaidi ni baba yupi ambaye nitazaa naye, wanaume wengi ni waluwalu tu,” alisema Maya.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini