
Vyanzo vyetu toka ndani ya jeshi la polisi vinasema kwamba, mama Wema alifika kituoni hapo Machi 19, mwaka huu na kutoa taarifa hiyo yenye kumbukumbu KJN/RB/2499/2014 na alihofu kuwa huenda hati hiyo iliibwa na wajanja wenye nia mbaya.
Ilidaiwa kuwa siku ya tukio saa nne usiku, mama huyo aliitafuta hati hiyo ili kesho yake akafungue madai ya mirathi ya mumewe lakini hakuiona mahali alipoiweka jambo lililomfanya aende polisi kuwajulisha.
Hati hiyo, kwa mujibu wa chanzo cha kipolisi hati hiyo ilitolewa katika Hospitali ya TMJ jijini Dar, Oktoba 27, mwaka jana.
Jumapili iliyopita, Uwazi lilimtafuta mama huyo ili kujua kama yeye ndiye aliyefikisha taarifa hizo polisi.
“Nililazimika kwenda huko kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee na sikuweza kujua kama aliyeichukua alikuwa na nia gani, lakini hata hivyo baada ya siku kadhaa kupita tangu nitoe taarifa niliitafuta tena nikakuta imerudishwa,” alisema mama Wema.
0 comments:
Post a Comment