LUPITA NYONG’O ASHINDA TUZO YA OSCAR YA ‘BEST SUPPORTING ACTRESS’

 
Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi, mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo ya Oscar ya mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''
Lupita+Nyong+o+86th+Annual+Academy+Awards+06nQ0wGEAoSl
Lupita+Nyong+o+Arrivals+86th+Annual+Academy+7fDugk2rpLDl
Lupita+Nyong+o+Arrivals+86th+Annual+Academy+Es2E157Urvdl
Nyong’o, 31, aliyeshinda tuzo ya Oscar kwenye filamu yake hiyo ya kwanza alipata shangwe za nguvu baada ya kutajwa kuwa mshindi. 


Amemshinda muigizaji mwenzie Jennifer Lawrence wa American Hustle” aliyekuwa akitajwa zaidi kuichukua tuzo hiyo. “Yes!” muigizaji huyo alisikika akisema wakati akipokea tuzo hiyo huku akimkumbatia kaka yake, muongozaji wa 12 Years a Slave, Steve McQueen na waigizaji wengine wa filamu hiyo.

Baada ya kupokea tuzo hiyo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''
 
Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''

Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini