IRENE PAUL: SIBAGUI DINI WALA KABILA KWENYE MAPENZI


Irene Paul.
MTOTO mzuri kwenye kilinge cha Bongo Movies, Irene Paul amefunguka kuwa kwenye suala la uhusiano, hana kipingamizi sana kwani anachoangalia ni mtu anayempenda haijalishi dini wala kabila.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni jijini Dar, Irene alisema licha ya kuwa bado hajamuanika mpenzi wake lakini suala la dini, kabila kwake siyo ishu ya msingi zaidi anaangalia mapenzi ya dhati.
“Naangalia tu, mtu anayenipenda ananipenda kweli au anaigiza? Nikigundua ananipenda kweli, nampenda pia. Hata aweje huyo ndiye atakayekuwa wangu wa maisha,” alisema Irene.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini