
STAA wa sinema za Kibongo, Flora Mvungi ameeleza masikitiko yake baada ya kuibiwa na vibaka.

Akizungumza na paparazi wetu, Flora alisema siku ya tukio mumewe H.
Baba alitoka na gari lake aina ya Toyota I.S.T kwenda mtaa wa
Lumumba-Kariakoo, akapaki na kuingia kwenye mizunguko yake lakini
aliporejea alishtuka baada ya kukuta kioo kimevunjwa na vitu
vilivyokuwemo ndani kuibiwa.

“Vibaka hawana maana wameiba laptop na vitu kibao vidogovidogo
ikiwemo flash iliyokuwa na nyimbo tano za mume wangu na wimbo mmojawapo
umeshavuja unaitwa Tubebane aliomshirikisha Mellon, inauma sana,”
alisema Flora.
0 comments:
Post a Comment