DINO AKACHA UIGIZAJI

Denis Swea ‘Dino’.
MKALI wa sinema za Kibongo, Denis Swea ‘Dino’ ameamua kuachana na uigizaji akidai haulipi.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni jijini Dar, Dino alisema badala ya kuigiza ameamua kurekodi vipindi ambavyo atavirusha katika televisheni kwani angalau inalipa kuliko sinema.
“Nimeona bora kuweka pembeni uigizaji na nimeelekeza nguvu zangu zote katika suala la kurekodi vipindi mbalimbali vya runinga, nitaangalia siku za usoni kama kuna haja ya kuigiza tena,” alisema Dino.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini