DIAMOND PLATNUMZ NI NOMA SANA



Katika mafanikio ya mtu maarufu,mengi husemwa na watu mbali mbali wengine,haswa pale msanii anapo-hustle kufanya kazi yake vizuri na hata kutambuika na fans wengi nje za nchi,hii yote inahitaji hard work,
kujituma bila ya kukata tama.Mafanikio ya msanii huwa yanapokelewa na watu tofauti kwa njia tofauti huku kila mtu anakuwa na lake la kusema,ila hizi ndizo tathmini zakushangaza zinazomuhusu Diamond Platnumz.



-Huyu ndio msanii wa kwanza Tanzania kushika namba moja katika moja ya chart za muziki duniani, katika stesheni ya kimataifa ya Trace ya nchini Ufaransa,lakini huko atokako nchini Tanzania kuna baadhi ya chart za muziki katika media, hayupo hata kwenye top 5.



-Ingawa inaonyesha wazi kuwa juhudi zake kimuziki ndio zinazofanya aweze ku-make headlines,kwa muziki wake kuzidi fanya vizuri hata kwa mataifa mengine yakigeni,baadhi ya watu wengi hapa tzee bado wanaamini kuwa muziki wake unahit kutokana na kuhonga kwake kwenye media ili nyimbo zake ziweze kupewa airtime.



-Akiwa kama mmoja wa watu maarufu sana hapa Tzee,Diamond ni msanii mkubwa sana, ila maisha yake ya kimahusiano yanaongelewa sana kwenye media kuliko celebrity yeyote yule hapa Tzee.



-Kwa umaarufu mkubwa aliokuwa nao kimuziki, huko nchini Nigeria na jinsi nyimbo zake zinavyopigwa mara kwa mara,haswa hii nyimbo yake ,remix ya Mynumber1 inavyozidi ku-make headline nchini humo na hata kwenye media nyingi za kimataifa,raia wengi wa nchini Nigeria wanadhani kuwa Diamond Platnumz ni raia wa nchini humo.



-ukiongelea wasanii wanaojiweza hapa town kupitia muziki tu,diamond platnumz hutaweza kumwacha,cause ni msanii anayeongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu sana katika show moja tu aifanyayo,jitihada zake kimuziki zimempelekea kuwa na utajiri mkubwa sana hapa town ila kuna baadhi ya mashabiki na watu wakawaida bado wanaamini kuwa huenda anajihusisha kuwa na madawa ya kulevya.

by OneloveTz

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Post a Comment

Ungana Nasi, Like Page Yetu Hapa Chini