MSANII wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amesema tabia mbaya za baadhi ya wasanii wenzao ndizo zinazowaharibia na kuwafanya wote waonekane hawana maadili.
Akiongea na GPL, Batuli alisema amekuwa akipata malalamiko kuwa
hawatumii katika filamu zake watoto Jenifer na Jamila waliokuwa
wakifanya kazi na marehemu Steven Kanumba, jambo ambalo amelikanusha.
“Siwezi kuwanyima watoto nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, sema watu
hawajui kilichopo nyuma ya pazia. Nimeshawahi kuwaita lakini wazazi wao
wakawazuia. Ilibidi nimchukue yule mtoto mwingine mvulana Patrick.
“Fikiri nafasi ya msichana inalazimishwa hadi anacheza mvulana ni
tatizo. Wasichokijua watu ni kwamba, wazazi wao wanawazuia wakiogopa
wataharibika. Wasanii tubadilikeni jamani,” alisema Batuli.
0 comments:
Post a Comment